• HABARI MPYA

    Monday, November 17, 2014

    WENGER AMTABIRIA BALLON D'OR PAUL POGBA NA ASEMA ALIMKOSAKOSA KIDOGO TU ALIPOKUWA MAN UNITED

    KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amemwagia sifa kede kede kinda Mfaransa, Paul Pogba akisema siku moja atakuwa Mwanasoka Bora wa Dunia, tena akiweka wazi alisotea sana saini ya mchezaji huyo.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alitemwa na Sir Alex Ferguson Man United mwaka 2012, na Wenger amesema alijaribu kumsajili kabla ya kwenda Juventus.
    Akizungumza na Televisheni ya Ufaransa, Wenger amesema: "Kama mwanasoka, yeye (Pogba) ana kila kitu. Ni vigumu kusema anakosa nini,".
    Sir Alex Ferguson alimuacha Pogba aondoke Old Trafford baada ya kucheza mechi tatu tu akitokea benchi.
    "Mambo yanakwenda haraka. Tulikuwa tuna nia naye. Tulijaribu kumpata aje hapa. Lakini akasaini haraka Juventus. Ana nafasi kubwa ya kushinda Ballon d'Or,"amesema Wenger. 
    Paul Pogba, pictured in France training on Sunday, has been a revelation for Juventus since signing in 2012
    Paul Pogba, pictured in France training on Sunday, has been a revelation for Juventus since signing in 2012
    Sir Alex Ferguson let Pogba leave Old Trafford having only made three substitute appearances
    Pogba in action for United in a Premier League match against West Brom

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER AMTABIRIA BALLON D'OR PAUL POGBA NA ASEMA ALIMKOSAKOSA KIDOGO TU ALIPOKUWA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top