• HABARI MPYA

    Monday, November 17, 2014

    WENGER AWACHARUKIA WAZUSHI NA KUWAPASHA; "PADOLSKI HAUZWI NA WALA HAONDOKI ARSENAL, YEYE AGOMBEE NAMBA TU"

    KOCHA wa Arsenal, Mfaransa Arsener Wenger amesema klabu hiyo haina mpango wa kumuuza mshambuliajinwake, Lukas Padolski. 
    Wenger amesistiza kwamba Podolski hatauzwa, licha ya taarifa kwamba mshambuliaji huyo wa Ujerumani anataka kuondoka katika klabu hiyo. 
    Bosi huyo wa amezipuuza habari zinazoandikwa mfululizo kwamba Podolski ataondoka Arsenal kwa dau la Euro Milioni 5 ifikapo Januari, kwa kusema; "Ni za kutengenezwa kabisa,". 
    Lukas Podolski aliichezea nchi yake dhidi ya Gibraltar wiki hii, lakini amekuwa akisotea namba Arsenal

    "Yeye (Podolski) hauzwi," Wenger amesema na kuongeza. "Mimi ndiye mtu ninayepanga bei, amerudi kutoka Kombe la Dunia, anacheza nafasi ambayo nina wachezaji wengine, anatakiwa kushindani namba,"amesema.
    Wenger amekanusha taarifa kwamba Podolski ataondoka Emirates, kwa kusema mshambuliaji huyo hauzwi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER AWACHARUKIA WAZUSHI NA KUWAPASHA; "PADOLSKI HAUZWI NA WALA HAONDOKI ARSENAL, YEYE AGOMBEE NAMBA TU" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top