• HABARI MPYA

    Sunday, November 16, 2014

    UNGETAMANI MAYWEATHER AWE BABA YAKO AKUPE ZAWADI HII KATIKA 'BETHIDEI' YAKO?

    BONDIA Floyd Mayweather ameendelea kutambia utajiri wake, baada ya kumnunuliwa mwanawe wa kiume, Karoun gari aina ya Bentley la rangi ya dhahabu maalum kwa ajili ya viwanja gofu.
    Mbabe huyo ambaye hajawahi kupoteza pambano, anafanya hivyo siku chache baada ya kuposti kwenye akaunti yake ya Instagram picha ya nori zenye thamani ya dola Milioni 100 mezani Ijumaa.
    Jumamosi, ameposti Bentley la kutembelea kwenye viwanja vya gofu ambalo ni zawadi kwa mwanawe, Koraun kwa ajili ya sherehe za miaka 15 ya kuzaliwa kwake!
    Floyd Mayweather poses for a photo with his  son Koraun on his birthday in his new gold Bentley golf cart
    Floyd Mayweather akiwa na kijana wake Koraun katika siku ya kuzaliwa wake na gari alilomnunulia 

    Wawili hao wanaonekana wakiwa pamoja kwenye gari lao katika kiwanja cha gofu kwenye picha hiyo na Mayweather ameambatanisha ujumbe kwenye Instagram usemao: "Kijana wangu @kingkoraun alitaka Bentley la gofu katika sherehe ya miaka 15 ya kuzaliwa kwake, hivyo nimemtimizia. Endelea kuangalia nitampa zawadi gani akitimiza miaka 16 ya kuzaliwa!'.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UNGETAMANI MAYWEATHER AWE BABA YAKO AKUPE ZAWADI HII KATIKA 'BETHIDEI' YAKO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top