MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mario Balotelli ameenguliwa kwenye kikosi cha Italia bada ya kuumia nyama mazoezini.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipata tatizo hilo katika mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Jumapili kufuzu Euro dhidi ya Croatia na ameshindwa kupata ahueni.
Iliamualiwa Jumamosi kwamba Balotelli ataruhusiwa kurejea kwenye klabu yake na Italia imetangaza rasmi kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Italia imethibitisha kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba Mario Balotelli ameondolewa kikosini baada ya kuumia
Balotelli hajafanikiwa kufunga bao tangu ajiunge Liverpool katika Ligi Kuu ya England msimu huu
Hilo ni pigo kubwa kwa mshambuliaji huyo wa Italia, ambaye amekuwa na wakati mgumu hadi sasa, akisotea kufanya vizuri tangu ahame AC Milan kwa dau la Pauni Milioni 16.
Balotelli angepata fursa nzuri ya kumshawishi kocha mpya, Antonio Conte katika mechi dhidi ya Croatia - hususan baada ya kutoitwa katika kikosi kilichopita.


.png)
0 comments:
Post a Comment