• HABARI MPYA

    Friday, November 07, 2014

    SPURS MAMBO SAFI EUROPA LEAGUE, YATOA KICHAPO UGENINI

    KLABU ya Tottenham Hotspur ya England imepata ushindi wa ugenini dhidi ya Asteras Tripolis katika mchezo wa Kundi C michuano ya Europa League.
    Ushindi huo unaifanya Spurs iikamate Besikitas kileleni mwa kundi hilo, zote zikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi nne. Asteras Tripolis inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake nne, wakati Partizan Belgrade yenye pointi moja inashika mkia.
    Andros Townsend aliifungia bao la kwanza Tottenham kwa penalti dakika ya 36 kabla ya 
    Harry Kane kufunga la pili dakika ya 42.
    Spurs ilipoteza mchezaji wake mmoja dakika za mwishoni, baada ya Federico Fazio kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Jeronimo Barrales kwenye boksi. Barrales aliifungia bao la kufutia machozi timu yake kwa penalti dakika ya 90.
    Kikosi cha Asteras Tripoli kilikuwa: Kosicky, Lluy, Sankare, Zisopoulos, Panteliadis, Usero, Munafo/Gianniotas dk81, Mazza, Rolle, Tsokanis/Badibanga dk60 na Parra/Barrales dk84. 
    Tottenham Hotspur: Vorm, Dier, Fazio, Vertonghen, Davies, Stambouli, Dembele, Townsend, Lamela/Soldado dk46, Eriksen/Mason dk63 na Kane/Paulinho dk77. 
    Harry Kane alifunga bao la ushindi Tottenham ikiilaza 2-1 Asteras Tipolis jana

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2824169/Asteras-Tripolis-1-2-Tottenham-Andros-Townsend-Harry-Kane-goals-strengthen-Spurs-grip-Europa-League-qualification.html#ixzz3IM90MaoC
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SPURS MAMBO SAFI EUROPA LEAGUE, YATOA KICHAPO UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top