• HABARI MPYA

    Friday, November 07, 2014

    EVERTON YABISHA HODI MTOANO ULAYA

    EVERTON imebisha hodi hatua ya mtoano ya Europa League kufuatia ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi H dhidi ya Lille ya Ufaransa Uwanja wa GoodisonPark, jana.
    Ushindi huo, unawafanya Toffees wafikishe pointi nane baada ya kucheza mechi nne ikipanda kileleni mwa kundi H, kwa kuizidi pointi moja, VfL Wolfsburg ya Ujerumani iliyo katika nafasi ya pili, wakati Lille inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu, huku FK Krasnodar yenye pointi mbili inashika mkia.
    Mabao ya Everton jana yalifungwa na Leon Osman dakika ya 27, Phil Jagielka dakika ya 42 na Steven Naismith dakika ya 61 katika mchezo ambao Samuel Eto’o na Steven Pienaar walibaki benchi muda wote.
    Kikosi cha Everton kilikuwa: Howard, Hibbert, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy/Besic dk85, Barry/Gibson dk67, Osman, Naismith, McGeady/Atsu dk66 na Lukaku. 
    Lille: Enyeama, Corchia/Rodelin dk75, Kjaer, Basa, Souare, Gueye, Mavuba, Balmont, Ryan Mendes/Beria dk64, Origi na Frey/Roux dk64.
    Leighton Baines wa Everton akipasua katikati ya wachezaji wa Lille, Simon Kjaer (kushoto) na Franck Beria

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2824399/Everton-3-0-Lille-Leon-Osman-Phil-Jagielka-Steven-Naismith-goals-Toffees-brink-Europa-League-knockout-stages.html#ixzz3IM4dvT9b 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EVERTON YABISHA HODI MTOANO ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top