TIMU ya taifa ya England imeichapa Slovenia mabao 3-1 katika mchezo wa Kundi D kufuzu Euro 2016 Uwanja wa Wembley, Nahodha Wayne Rooney akizawadiwa 'kofia ya dhahabu' baada ya kuwa mchezaji mdogo aliyetimiza mechi 100 kihistoria England.
Nahodha wa Slovenia, Bostjan Cesar alikuwa mwenye bahati kwa kutopewa kadi nyekundu baada ya kumpiga usoni Adam Lallana katika mchezo ambao, England walifungwa bao la kwanza katika kampeni hizo za kufuzu, baada ya Jordan Henderson kujifunga kipindi cha pili.
Nahodha Rooney aliisawazishia kwa penalti baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu akifunga bao lake la 44 timu ya taifa.
Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck akafunga mabao mawili ndani ya dakika sita kuihakikishia England ushindi huo na rekodi safi.
Kikosi cha England kilikuwa; Hart, Clyne, Cahill, Jagielka, Gibbs, Henderson, Wilshere, Lallana/Milner dk6, Welbeck, Rooney na Sterling/Oxlade-Chamberlain.
Slovenia: Handanovic, Brecko, Ilic, Cesar, Sturna, Mertelj, Kurtic/Rotman dk75, Birsa/Lazarevic dk63, Kampl, Kirm/Ljubijankic dk78 na Novakovic.
Wayne Rooney akipunga mkono angani baada ya kufunga kwa penalti
Danny Welbeck akiifungia England leo
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2836035/England-3-1-Slovenia-Wayne-Rooney-marks-century-equaliser-Danny-Welbeck-double-sees-Three-Lions-roar-finals.html#ixzz3JAbzrQ4w


.png)
0 comments:
Post a Comment