• HABARI MPYA

    Sunday, November 16, 2014

    ISCO ACHEKA NA NYAVU HISPANIA IKIIRARUA 3-0 BELARUS KUFUZU EURO 2016

    HISPANIA imeichapa mabao 3-0 Belarus katika mchezo wa Kundi C kufuzu Kombe la Mataifa ya Ulaya usiku huu.
    Kiungo wa Real Madrid, Isco aliifungia Hispania bao la kwanza dakika ya 18 kabla ya nyota wa Barcelona, Sergio Busquets kufunga la pili dakika moja baadaye.
    Dakika 10 baada ya kuanza kipindi cha pili, Pedro akawafungia mabingwa hao watetezi wa Ulaya bao la tatu na sasa Hispania inapanda nafasi ya pili katika Kundi C.Kikosi cha Hispania kilikuwa; Casillas, Juanfran, Pique, Ramos, Alba, Cazorla/Callejon dk69, Busquets/Bruno dk45, Koke, Isco/Morata dk80, Pedro na Alcacer.
    Belarus: Zhevnov, Matsveychyk, Politevich, Martynovich/Bordachev dk31, Yanushkevich, Balanovich, Kalachev, Dragun, Nekhaychik, Krivets/Kislyak dk80 na Kornilenko/Signevich dk67.
    Spain's Isco (left) celebrates with Jordi Alba (right) and Koke after putting his side ahead against Belarus in Huelva
    Nyota wa Hispania, Isco (kushoto) akishangilia na Jordi Alba (kulia) na Koke baada ya kuifungia bao timu yake hiyo ya taifa usiku huu dhidi ya Belarus mjini Huelva

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2836109/Spain-3-0-Belarus-Isco-nets-stunner-Sergio-Busquets-Pedro-scored-easy-win-European-champions.html#ixzz3JB612tsq 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ISCO ACHEKA NA NYAVU HISPANIA IKIIRARUA 3-0 BELARUS KUFUZU EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top