• HABARI MPYA

    Saturday, November 15, 2014

    RANIERI ATIMULIWA UGIRIKI BAADA YA KIPIGO CHA VIBONDE FAORES ISLANDS KUFUZU EURO 2016

    Ranieri amefukuzwa kazi Ugiriki
    KOCHA Claudio Ranieri leo amefukuzwa kazi Ugiriki kufuatia kipigo cha 1-0 nyumbani mbele ya vibonde Faroes Islands katika mchezo wa kufuzu Euro 2016.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Ugiriki limsema kocha huyo Mtaliano mwenye umri wa miaka 63 atabakia nchini humo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Serbia Jumanne kabla ya kurejea kwao.
    Kipigo hicho cha Faroes kinawaacha mabingwa hao wa zamani wa Ulaya, Ugiriki mkiani mwa Kundi F na kujiweka katika nafasi finyu ya kufuzu Euro 2016 nchini Ufaransa.
    Taarifa imesema kwamba uamuzi wa kutimuliwa kwa Ranieri ulifikiwa kikao kilichohudhuriwa na Rais Giorgos Sarris. "Hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kuvunja Mkataba,"imesema taaruifa hiyo, ikisistiza sababu ni kipigo cha Faroes.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RANIERI ATIMULIWA UGIRIKI BAADA YA KIPIGO CHA VIBONDE FAORES ISLANDS KUFUZU EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top