![]() |
| Hayatou kulia akiwa na Jamal Malinzi, rais wa TFF |
"Tunakwenda kubaki katika msingi wa sheria, ambayo inamaanisha kuondolewa katika michuano miwili ya Mataifa ya Afrika," Hayatou amesema akizungumza na gazeti la michezo la Ufaransa la kila siku, L'Equipe na kuongeza; "Na juu ya halo watapigwa faini ya fedha,".
Morocco wanakabikiwa na faini ya cola za KImarekani Milioni 20 kwa kughairi kuwa wenyeji wa AFCON ya 2015 inayotarajiwa kuanza Januari 17 hadi Februari 8, baada ya kugoma kwa sababu ya kuhofia ugongwa wa Ebola.
Matajiri wa mafuta, Equatorial Guinea, ambao waliandaa kwa pamoja na Gabon AFCON ya 2012 walitajwa kuchukua nafasi ya Morocco ya uenyeji wa michuano hiyo jana ingawa wanakabiliwa na ushindani wa Tunisia, Algeria na Cape Verde.



.png)
0 comments:
Post a Comment