Na Mwandishi Wetu, MAPUTO
NDOTO za Msumbiji kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zimedidi kuyeyuka jioni ya leo baada ya kufungwa nyumbani 1-0 na Zambia katika mchezo wa Kundi F, Uwanja wa Taifa, wa Zimpeto, Maputo.
Bao lililoizamisha Mambas iliyofuzu dhidi ya Tanzania kwa mbeleko ya refa wa Uganda, Dennis Batte kupata nafasi kuingia kwenye kundi hilo, lilifungwa na Given Singuluma dakika ya 67.
Matokeo haya yanamaanisha, Chipolopolo iliyofikisha pointi nane baada ya mechi tano ina nafasi ya kuungana na vinara wa kundi, Cerpe Verde wenye pointi tisa kufuzu AFCON.
Msumbiji inayobaki na pointi zake tano baada ya mechi tano pia kwa pamoja na Niger yenye pointi mbili hazina nafasi ya kwenda AFCON.
Katika mechi nyingine zao leo, Togo imefumuliwa mabao 4-1 nyumbai na Guinea Uwanja wa Kegue. Mabao ya Guinea yamefungwa na Idrissa Sylla dakika ya 25 na Seydouba Soumah aliyefunga matatu dakika za 40, 59 na 65 wakati bao pekee la Togo limefungwa na Emmanuel Adebayor dakika ya 69.
Angola imetoka 0-0 na Gabon, wakati mabao ya Kalu Uche kwa penalti dakika ya 59 na Aaron Samuel Olaare dakika ya 90 yameipa Nigeria ushindi wa 2-0 dhidi ya Kongo uwanja wa Manispa na Cameroon imeilaza 1-0 DRC, bao pekee la Vincent Aboubakar dakika ya 71.
Lesotho imelala 1-0 nyumbani mbele ya Burkina Faso, bao pekee la Jonathan Pitroipa. Mechi nyingine zilizochezwa mapema jioni ya leo, bao pekee la Savio Kabugo dakika ya tisa, limeipa Uganda ushindi wa 1-0 Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, dhidi ya Ghana.
Afrika Kusini imeilaza 2-1 Sudan Uwanja wa Moses Mabhida, mechi ya Kundi A mabao ya Bafana Bafana yakifungwa na Thulani Serero dakika ya 38 na Tokelo Rantie dakika ya 53, wakati bao pekee la Sudan limefungwa na Salah Ibrahim dakika ya 77.
Malawi imepata ushindi wa 2-0 dhidi ya Mali Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, mabao ya Robert Ng'ambi dakika ya 64 na Esau Kanyenda dakika ya 85.
Mechi za jana, Botswana ilitoka 0-0 na Tunisia Uwanja wa Taifa wa Gaborone, mchezo wa Kundi G, wakati Ivory Coast ilipata ushindi mzuri ugenini wa 5-1 dhidi ya Sierra Leone.

![]() |
| Msumbiji wamefungwa 1-0 Maputo leo |

.png)
0 comments:
Post a Comment