• HABARI MPYA

    Sunday, November 16, 2014

    KLITSCHKO AMKALISHA KUBRAT ULEV MARA TATU KABLA YA KUMLAZA MOJA KWA MOJA RAUNDI YA TANO NA KUTETEA MATAJI WAKE YA DUNIA

    BONDIA Wladimir Klitschko amefanikiwa kutetea kwa mara ya 17 mfululizo taji lake, baada ya kumpiga Knockout Kubrat Pulev Raundi ya tano mjini Hamburg jana usiku.
    Bingwa huyo wa uzito wa juu wa IBF, WBA na WBO alimbwaga chini mara mbili mpinzani wake katika raundi ya kwanza na ikaonekana kama pambano hilo halitafika mbali.
    Pulev aliangushwa chini tena katika raundi ya tatu, lakini tena akafanikiwa kuinuka kabla ya kukutana na ngumi ya mkono wa kushoto ya Klitschko raundi ya tano na kumfanya Mbulgaria huyo apoteze pambano la kwanza baada ya kupanda ulingoni mara 21 na Klitschko kuendeleza rekodi yake ya kushinda mapambano 63 na kupoteza matatu, 53 kati ya hayo kwa Knockout.
    The Ukrainian retained his IBF world heavyweight title with a fifth-round victory in Germany
    Mbabe wa Ukraine ametetea taji lake la IBF uzito wa juu kwa ushindi wa raundi ya tano nchini Ujerumani
    Klitschko put his Bulgarian opponent on the floor four times in five rounds in Hamburg
    Klitschko akimkalisha Mbulgaria mjini Hamburg

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-2836209/Wladimir-Klitschko-retains-IBF-heavyweight-title-devastating-fifth-round-knockout-Bulgarian-Kubrat-Pulev-Hamburg.html#ixzz3JDGWJLun 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KLITSCHKO AMKALISHA KUBRAT ULEV MARA TATU KABLA YA KUMLAZA MOJA KWA MOJA RAUNDI YA TANO NA KUTETEA MATAJI WAKE YA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top