• HABARI MPYA

    Sunday, November 16, 2014

    JOE HART AENGULIWA KIKOSINI ENGLAND

    KIPA Joe Hart amepewa mapumziko katika timu ya soka ya taifa ya England na hatakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Scotland Jumanne- akimpa nafasi Fraser Forster kuichezea nchi yake katika Uwanja wa klabu yake ya zamani, Celtic Park.
    Kocha wa Three Lions, Roy Hodgson amesema amemuacha Hart nje ya kikosi cha kucheza mechi hiyo ya Glasgow baada ya kipa huyo namba moja wa Manchester City kuisaidia England kuifunga Slovenia 3-1 Jumamosi.
    Hodgson amesema: "Ninamruhusu Leighton Baines kwenye mchezo na Scotland, lakini pia ni majeruhi,".Joe Hart clears the ball during England's Euro 2016 qualifier against Slovenia at Wembley Stadium
    Joe Hart akimpiga mpira wakati England ikicheza na Slovenia kwenye mechi ya Euro 2016 Uwanja wa Wembley

    "Mwingine ni Joe Hart. Atakwenda nyumbani kupumzika kwa sababu nina makipa wengine wawili naweza kuwachezesha. 
    Forster aliwahi kuichezea Celtic kabla ya kuhamia Southampton na kipa mwingine kwenye kikosi cha Hodgson ni Ben Foster wa West Brom.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JOE HART AENGULIWA KIKOSINI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top