• HABARI MPYA

    Monday, November 17, 2014

    BOBAN AMPOROMOSHEA MANENO MAKALI FELLAINI, AMUAMBIA; "HUWEZI KUCHEZA SOKA"

    NYOTA wa zamani wa AC Milan na Croatia, Zvonimir Boban amemkandia kiungo wa Manchester United, Marouane Fellaini, akisema kwamba mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 27.5 hawezi kucheza soka.
    Kauli hiyo aliitoa baada ya mchezo wa jana kufuzu Euro kati ya Ubelgiji na Wales timu hizo zikitoka sare ya bila kufungana.
    Fellaini, ambaye alicheza dakika zote 90 kikosi cha Ubelgiji dhidi ya Wales ya Chris Coleman, alizua tafrani baada ya kumpiga usoni mchezaji wa Liverpool, Joe Allen.
    Kiungo huyo wa United alinusurika kupewa kadi na refa Pavel Kralovec, lakini hajaweza kuepuka maneno ya Boban akimkandia hadharani baada ya tukio hilo.

    Marouane Fellaini, pichani akimpiga Joe Allen, tukio ambalo limemkera Zvonimir Boban na kusema hawezi soka
    As the pair tangled, Fellaini landed a dangerous elbow to the face of Wales midfielder Allen
    Allen's head was flung back, and the midfielder left the field temporarily bloodied
    Fellaini akimchezea kindava kiungo wa Wales, Allen katika mchezo huo kipindi cha pili

    Nyota wa zamani wa AC Milan na Croatia, Boban hamfagilii nyota wa United, Fellaini

    Boban, ambaye aliichezea AC Milan kwa miaka 11 na kushinda nayo mataji manne ya Serie A na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya amesema: "Fellaini hawezi kucheza soka. Kabisa hawezi kucheza soka," amenukuliwa na Daily Mirror:
    Kiungo huyo wa zamani wa Yugoslavia na Croatia anamkandia  Fellaini wakati mambo yameanza kumnyookea katika kikosi cha kwanza cha United baada ya kupona kifundo cha mguu.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa na namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Louis van Gaal tangu atokee benchi na kufunga bao lake la kwanza katika mechi ya mashindano dhidi ya West Brom katika klabu hiyo.
    Fellaini alikuwa ana wakati mgumu Old Trafford msimu uliopita kabla ya mambo kuanza kumnyookea  baada ya kuondoka kwa kocha David Moyes. Nyota huyo wa zamani wa Everton anatarajiwa kuanza pia katika mechi dhidi ya Arsenal mwishoni mwa wiki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BOBAN AMPOROMOSHEA MANENO MAKALI FELLAINI, AMUAMBIA; "HUWEZI KUCHEZA SOKA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top