Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MLINDA mlango wa pili wa Simba SC, Hussein Sharrif ‘Casillas’ kesho anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi baada ya kutoa nyuzi alizoshonwa kwenye ugoko kufuatia kuumia mwezi uliopita.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni ya leo, Casillas amesema kwamba baada ya kufungua nyuzi hizo za chuma sasa anaweza kuanza mazoezi, kama ya gym na kukimbia mchangani.
“Ninaanza mazoezi ya peke yangu baada ya kufungua nyuzi, natarajia Mungu atanijaalia nitakuwa fiti tena na kurejea uwanjani,”amesema Cassilas, ambaye aligongwa kwa kiatu chenye ‘njumu’ za chuma na mchezaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini na kuchanika vibaya ugoko wake.
Casillas alitolewa mwishoni mwa kipindi cha kwanza Oktoba 11, mwaka huu akiidakia Simba SC katika mchezo wa kirafiki uliomalizika kwa sare ya bila kufungana baada ya kuumia, nafasi yake ikichukuliwa na kipa wa tatu, Peter Manyika.
Casillas aliumia wakati Simba SC imeweka kambi ya wiki moja na ushei Afrika Kusini kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC uliofanyika Oktoba 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Casillas aliyefanyiwa upasuaji wa kiwango cha juu, kuungwa ugoko wake uliopasuka na baadaye kushonwa kwa nyuzi ngumu mfano wa waya, alitakiwa kupumzika kwa wiki sita.
Casillas amesajiliwa Simba SC msimu huu akitokea
Mtibwa Sugar ya Morogoro aliyoanza kuichezea mwaka 2010 akitokea Villa Squad ya Dar es Salaam.
Kipa huyo mwenye tuzo mbili hadi sasa, Kipa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita na kipa bora wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA) mwaka jana, amesema anatarajia mapema Desemba ataanza mazoezi kikamilifu na klabu yake.

![]() |
| Hussein Sharrif 'Casillas' akiwa na tuzo zake mbili |
![]() |
| Eneo la ugoko wa Casillas baada ya kutolewa nyuzi |
Casillas aliumia wakati Simba SC imeweka kambi ya wiki moja na ushei Afrika Kusini kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC uliofanyika Oktoba 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Casillas aliyefanyiwa upasuaji wa kiwango cha juu, kuungwa ugoko wake uliopasuka na baadaye kushonwa kwa nyuzi ngumu mfano wa waya, alitakiwa kupumzika kwa wiki sita.
Casillas amesajiliwa Simba SC msimu huu akitokea
Mtibwa Sugar ya Morogoro aliyoanza kuichezea mwaka 2010 akitokea Villa Squad ya Dar es Salaam.
Kipa huyo mwenye tuzo mbili hadi sasa, Kipa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita na kipa bora wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA) mwaka jana, amesema anatarajia mapema Desemba ataanza mazoezi kikamilifu na klabu yake.

.png)
0 comments:
Post a Comment