MSHAMBULIAJI kinda wa Arsenal, Yaya Sanogo au Yaya Sanogoal amwfunga mabao manne katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Benfica jioni hii mchezo wa ufunguzi Kombe la Emirates.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye alianza kucheza England msimu uliopita akipewa mechi 14 mashindano tote alifunga mabao hayo katika dakika za
26, 44, 45 na ushei na 49, wakati bao lingine la Gunners lilifungwa na Joel Campobell.
Bao pekee la kufutia machozi la timu a Ureno lilifungwa na Gaitan dakika ya 62.
Shoo la mtu mmoja: Yaya Sanogo ameifungia mabao manne Arsenal katika ushindi wa 5-1 Kombe la Emirates dhidi ya Benfica
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Martinez, Bellerin, Chambers, Monreal/Miquel dk73, Gibbs, Flamini/Arteta dk60, Campbell/Sanchez dk73, Ramsey/Wilshere dk60, Rosicky/Coquelin dk60, Oxlade-Chamberlain/Cazorla dk46 na Sanogo/Akpom dk73.
Benfica: Artur, Amorim/Joao Teixeira dk85, Gaitan/Cancelo dk85, Lima/Derlei dk85, Maxi Pereira, Ola John/Candeias dk60, Salvio/Bebe dk57, Eliseu/Benito dk19, Sidnei, Talisca/Andre Almeida dk60 na Cesar.
Sanogo (kulia) akiifungia Arsenal bao la kwanza
0 comments:
Post a Comment