WACHEZAJI watatu wa timu ya pili ya Yanga SC, ama timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu Yanga B walikuwemo katika kikosi cha timu hiyo kilichotwaa Kombe la Kagame mwaka 2012, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mjini Dar es Salaam.
Hao ni viungo Issa Ngao, Frank Domayo na Simon Msuva, wakati huo timu hiyo ikifundishwa na kocha Mbelgiji, Tom Saintfiet ambaye kwa sasa yupo Free State Stars ya Afrika Kusini.
Msuva na Domayo walikuwa ndiyo kwanza wanasajiliwa wakati Ngao alikuwemo kwenye U20 ya Yanga tangu msimu uliotangulia.
Yanga SC iliwasajili wachezaji hao kama wa timu B, kwa kuwa wakati huo pia walisajiliwa kama wachezaji wa timu za vijana za klabu walizotoka, Msuva Moro United na Domayo JKT Ruvu.
Lakini pia, walikuwa bado wana umri chini ya miaka 20 na kutokana na ujanja au maarifa ya kisoka aliyokuwa nayo Katibu wa wakati huo wa klabu hiyo, Celestine Mweisgwa alifanya hivyo ili kuiongezea klabu nafasi za kusajili wachezaji wapya wa wa kikosi cha kwanza.
Kanuni za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zinasema mchezaji anayesajiliwa kikosi cha U20, anaweza pia kucheza Ligi Kuu.
Tena timu inaweza kupanga kikosi kizima cha U20 katika mchezo wa Ligi Kuu ikiamua- tumeona wakati fulani Simba SC ilitumia vizuri fursa hiyo kuinua vipaji vya yosso yao kama akina Ramadhani Singano ‘Messi’, Haroun Chanongo, Abdallah Seseme, William Lucian ‘Gallas’, Said Ndemla, Hassan Hatibu na wengineo.
Baraza la Vyama Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) liliishuhudia Yanga SC ikicheza mechi ya kwanza hadi ya mwisho ya Kagame 2012 hadi kutwaa ubingwa.
Mwaka jana, Yanga SC hawakwenda Sudan kutetea Kombe kutokana na hofu ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyokuwa yakiendelea nchini humo na Vital’O ya Burundi ikarithi taji hilo.
Kwa kuwa mabingwa wa msimu wa 2012/2013, Yanga walitakiwa kuwapo katika michuano ya Kagame mwaka huu mjini hapa, Kigali, Rwanda.
Lakini badala yake sasa, Tanzania Bara inawakilishwa na Azam FC waliokuwa washindi wa pili msimu huo.
Hiyo inafuatia CECAFA kuigomea Yanga SC kuja kushiriki, baada ya Sekretarieti ya sasa kupeleka kikosi cha pili, kilichoongezewa nguvu na wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza.
Kocha wa Yanga B, Nsajigwa Shadrack angekuja Rwanda kuiongoza timu, wakati Makocha wa timu A, Wabrazil Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Leiva wangeendelea kuiandaa timu ya kwanza kwa msimu wa Ligi Kuu nyumbani.
CECAFA ikawapa muda Yanga SC kubadilisha aina ya kikosi walichokileta badala yake wapeleke timu A, na waliposhindwa kufanya hivyo ndani ya muda, wakaiagiza TFF iteue timu nyingine ya kuchukua nafasi hiyo.
Azam FC wamechukua nafasi hiyo ya Yanga SC na sasa wapo Robo Fainali, hatua mbili kuelekea mwisho wa mashindano.
Lakini baada ya mashindano kuanza mjini hapa, ikagundulika timu kadhaa zimeleta wachezaji vijana wadogo jambo ambalo limeungwa mkono hadi na Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye.
Musonye amefurahia timu kama APR, Rayon, Merreikh na nyingine kuja na vijana wadogo zaidi katika vikosi vyao- akiamini zinaandaa nyota wa baadaye.
Hilo limewauma sana Yanga SC na sasa wanaona kama wao walionewa, kwa sababu pia walitaka kuja na kikosi mchanganyiko chenye wachezaji wengi vijana wadogo na kocha wa timu B.
Kweli, baadhi ya timu hapa zina wachezaji wenye sura changa mno, amnao wanaonyesha vipaji- lakini hakuna timu hata moja hapa ambayo imekuja na benchi la Ufundi la timu B.
CECAFA isingekuwa na neno na Yanga SC, kama kocha Maximo angekuja na wachezaji wale wale ambao klabu ilitaka wacheze mashindano hayo- lakini kitendo cha kutaka kuleta ile timu ambayo ilitolewa hatua ya 16 Bora mchuano ya Rollingston mwezi uliopita Dar es Salaam ndiyo kilikuwa tatizo.
Mapema kabisa mwanzoni mwa mashindano baadhi ya viongozi wa CECAFA walizungumzia mpango wa kuiadhibu Yanga SC kwa kitendo hicho- sijui kama mpango huu upo tena baada ya kubainika Ethiopia imeleta timu isiyo ya Ligi Kuu, Adama City.
Lakini viongozi wa Yanga SC hawapaswi kuishia kulalamika kwenye vyombo vya Habari, wanatakiwa kutuma malalamiko yao kiofisi, kimaandishi kwa CECAFA.
Wahoji sababu za msingi za wao kuondolewa kwenye mashindano, wakati timu nyingine zimeleta ‘watoto wengi’ na Ethiopia wamewakilishwa na timu isiyo ya Ligi Kuu.
Naamini, CECAFA watawapa ufafanuzi Yanga SC na huo utakuwa mwanzo mzuri wa kumaliza tatizo lililojitokeza, ili klabu hiyo isiadhibiwe.
CECAFA ni mwanachama halali wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambaye anaweza kabisa kuiponza Yanga SC kufungiwa kucheza michuano ya Afrika, iwapo watapeleka taarifa mbaya juu ya klabu hiyo.
Ilitokea kwa mchezaji Tressor Mputu wakati akiichezea TP Mazembe ya DRC, alifungiwa na CECAFA mwaka mzima kwa utovu wa nidhamu Kombe la Kagame mjini hapa, Kigali na akafungiwa pia kucheza michuano ya CAF.
Yanga SC wenyewe baada ya kugomea mchezo wa mshindi wa tatu wa Kombe kla Kagame mwaka 2009 dhidi ya Simba SC, iliponea chupuchupu kufungiwa miaka miwili kucheza mashindano ya CECAFA na CAF, wakatozwa faini dola za Kimarekani 20,000.
Kwa hivyo, viongozi wa Yanga SC wasileweshwe na mijadala ya kwenye mabaraza ya kahawa, kwamba CECAFA si lolote, hapana- wachukue hatua zaidi za kiofisi kuweka mambo sawa.
Kwa sababu mlolongo mzima wa Yanga SC kuondolewa kwenye mashindano, unaanzia kwa wao wenyewe.
Kocha wao Maximo, alisema timu yake haiko tayari kwa mashindano, kwa kuwa baadhi ya wachezaji waliokuwa na timu za taifa hakuawahi kufanya nao mazoezi kabisa tangu amekuja nchini.
Akasema asingekuwa tayari kuja Rwanda na timu ambayo wachezaji wengi hawajui- hivyo akashauri iende timu B na baadhi ya wachezaji wa timu A- hayo yalikuwa matatizo yao wenyewe Yanga SC, hayakuihusu CECAFA wala kanuni za mashindano ya Kagame na ukichanganya na mawasiliano mabovu baina yao, ikawa ilivyokuwa. Alamsiki.

0 comments:
Post a Comment