 |
| Ronaldo |
NYOTA wa zamani wa Brazil, Ronaldo, Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi
ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, jana ameonyesha nia yake ya kuwa rais
wa Shirikisho la Soka la nchi yake.
"Ningependa kufanya siasa zangu katika soka. Nataka
kuwa mwanasiasa wa soka,"alisema.
Ronaldo, ambaye alitwaa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha
Brazil mwaka 2002, hafahamu kama atagombea nafasi hiyo, lakini CBF ikimtaka
atakubali.
0 comments:
Post a Comment