• HABARI MPYA

    Friday, March 08, 2019

    AMUNIKE AWAKAUSHIA AJIBU, DILUNGA KIKOSI CHA STARS KITAKACHOIVAA UGANDA KUFUZU AFCON

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Tanzania, Mnigeria Emmanuel Amunike hajawaita viungo Ibrahim Ajibu wa Yanga na Hassan Dilunga wa Simba SC katika kikosi cha Taifa Stars kitakachomenyana na Uganda katika mchezo wa mwisho wa Kundi L kufuzu Fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Machi 24, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Amunike pia amewaacha beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye amekuwa katika kiwango kizuri siku karibuni pamoja na kipa chipukizi wa Yanga, Ramadhani Kabwili.
    Amewaita wachezaji wote watatu wanaocheza Misri, viungo; Himid Mao wa Petrojet FC, Shiza Kichuya anayecheza kwa mkopo ENPPI kutoka Pharco FC ya huko pia na mshambuliaji Yahya Zayd wa Ismailia.
    Emmanuel Amunike hajamuita Nahodha wa Yanga, Ibrahim Ajibu katika kikosi cha Taifa Stars kitakachoivaa Uganda mwishoni mwa mwezi huu

    Taifa Stars itakuwa mwenyeji wa The Cranes Jumapili ya Machi 24 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), siku ambayo Cape Verde watawakaribisha Lesotho Uwanja wa da Varzea mjini Praia katika mchezo mwingine wa kundi hilo. 
    Tanzania inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kujitengenezea mazingira ya kufuzu AFCON ya kwanza tangu mwaka 19980 nchini Nigeria.
    Lakini pia Watanzania watatakiwa kuiombea dua mbaya Lesotho isishinde mbele ya Cape Verde mjini Praia, kwani ikishinda itafuzu kutokana na wastani wake mzuri wa mabao na pia kubebwa kwa matokeo yake dhidi ya Taifa Stars.
    Kikosi kamili cha Taifa Stars; Makipa; Aishi Manula (Simba SC), Aaron Kalambo (Tanzania Prisons) na Metacha Mnata (Mbao FC).
    Mabeki; Suleiman Salula (Malindi SC), Hassan Kessy (Nkana FC - Zambia), Gardiel Michael (Yanga SC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Vincent Philipo (Mbao FC), Ally Mtoni ‘Sonso’ (Lipuli FC), Andrew Vincent ‘Dante’ (Yanga SC), Kennedy Wilson (Singida United) na Aggrey Morris (Azam FC). 
    Viungo; Feisal Salum (Yanga SC), Jonas Mkude (Simba SC), Himid Mao (Petrojet FC - Misri), Mudathir Yahya (Azam FC), Shiza Kichuya (ENPPI - Misri), Simon Msuva (Difaa El Jadida – Morocco) na Farid Mussa (Tenerife B).
    Washambuliaji; Yahya Zayd (Ismailia - Misri), Shaaban Iddi Chilunda (CD Izara – Hispania), Rashid Mandawa (BDF XI - Botswana), Thomas Ulimwengu (JS Saoura - Algeria), John Bocco (Simba SC) na Mbwana Samatta (KRC Genk – Ubelgiji).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMUNIKE AWAKAUSHIA AJIBU, DILUNGA KIKOSI CHA STARS KITAKACHOIVAA UGANDA KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top