• HABARI MPYA

  Thursday, October 04, 2018

  AMBOKILE WA MBEYA CITY AWA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU SEPTEMBA AWAFUNIKA AJIBU NA MBONDE

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa timu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya, Eliud Ambokile (pichani kushoto) amechaguliwa kuwa mchezaji wa mwezi Septemba wa Ligi kuu Tanzania Bara.
  Ambokile anakuwa mchezaji bora wa pili wa mwezi katika msimu mpya wa Ligi Kuu, baada ya mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere wa Simba SC kuwa mchezaji bora wa Agosti.  
  Kamati ya tuzo ya wachezaji bora Ligi Kuu Tanzania Bara imemtangaza mchezaji huyo mwenye jumla ya magoli 6 akiwa ndo kinara wa wafungaji wa Ligi hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Ibrahim Ajib wa Yanga na Stahmili Mbonde wa Mtibwa Sugar.
  Katika mwezi huo Ambokile alionyesha uwezo mkubwa uwanjani ikiwa ni pamoja ya kufunga magoli manne ambapo timu yake ilishinda michezo miwili na sare moja na kupoteza michezo miwili.
  Ajibu yeye aliisaidia timu yake kushinda michezo mitatu na sare moja huku mbonde akiisaidia timu yake kushinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza mmoja.
  Ambokile atazawadiwa tuzo na shilingi milioni moja pamoja na kisimbusi cha Azam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMBOKILE WA MBEYA CITY AWA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU SEPTEMBA AWAFUNIKA AJIBU NA MBONDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top