• HABARI MPYA

  Saturday, June 09, 2018

  PATAMU TAIFA LEO ‘TEAM SAMATTA V TEAM KIBA’ KATIKA MECHI YA HISANI KUCHANGIA VIFAA NA MIUNDOMBINU YA SHULE

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kirafiki wa Hisani utakaohusisha nyota mbalimbali wa soka wakiwemo wastaafu wakiongozwa na Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta na Mwanamuiki nyota nchini, Ali ‘King’ Kiba unafanyika leo jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana mjini Dar es Salam, Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, amesema kwamba mchezo huo uliopewa jina #Nifuate ni wa kuhamasisha uchangiaji wa vifaa na miundombinu mashuleni utakuwa ni baina yeye na rafiki zake dhidi ya mwanamuziki Ali Kiba na rafiki zake.  

  “Ni mechi ya hisani ya Samatta 11 na Ali Kiba 11, nimechagua rafiki zangu na Ali amechagua rafiki zake. Ni mechi ya Hisani kama nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikifanywa na wachezaji wakubwa,”alisema Samatta ambaye amewataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwa sababu kutakuwa na burudani nyingine pia. 
  Kwa upande Ali Kiba amesema kwamba amefurahi sana urafiki wake na Samatta kuzalisha kitu hicho kizuri na amewaomba wapenzi na mashabiki wake kujitokeza kwa wingi Uwanja leo kwenye mchezo huo wa Hisani ambao mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison George Mwakyembe.
  Samatta atakuwa anacheza kwa mara ya kwanza nje ya Taifa Stars tangu aondoke Simba SC mwaka 2011 kwenda TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambayo ilimuuza Genk mwaka juzi – na King ataonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu aoe mwezi uliopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PATAMU TAIFA LEO ‘TEAM SAMATTA V TEAM KIBA’ KATIKA MECHI YA HISANI KUCHANGIA VIFAA NA MIUNDOMBINU YA SHULE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top