• HABARI MPYA

  Tuesday, June 12, 2018

  MWAMBUSI ATUA AZAM FC KUWA KOCHA MSAIDIZI WA PLUIJM

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imeendelea kujiumba upya kwa ajili ya msimu ujao, baada ya leo kuingia mkataba wa miaka miwili na kocha wa zamani wa, Yanga SC Juma Mwambusi. 
  Kocha huyo Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2013-2014 akiwa na Mbeya City ya nyumbani kwao, Mbeya anakwenda kuungana tena na Mholanzi, Hans van der Pluijm ambaye naye amejiunga na Azam FC mwezi huu kama Kocha Mkuu mpya.
  Wawili hao walifanya kazi kwa maelewano mazuri na kwa mafanikio makubwa kwa misimu miwili Yanga SC, 2015-2016 na 2016-2017 wakitwaa ubingwa wa Ligi Kuu mfululizo kabla ya wote kuondolewa kupisha benchi jipya la Ufundi chini ya Mzambia, George Lwandamina ambaye naye tayari ameondoka.

  Meneja wa Azam FC, Philipo Alando (kulia) akibadilishana mikataba na kocha Juma Mwambusi baada ya kusaini

  Wakati Pluijm alikwenda Singida United baada ya kuondoka Yanga, Mwambusi aliamua kupumzika kwa muda wote huo hadi sasa anaibukia Azam FC.
  Tayari Azam FC imekwishamtangaza Pluijm kuwa kuwa kocha wake mpya, akichukua nafasi ya Mromania, Aristica Cioaba aliyeondolewa baada ya matokeo mabaya msimu huu. 
  Pluijm alikuja Tanzania mwaka 2014 na kujiunga na Yanga SC alikofanya kazi kwa msimu mmoja kabla ya kwenda Al Shoalah FC ya Saudi Arabia na kurejea Jangwani mwaka 2015 akafanya kazi Novemba 2016 alipohamia Singida United.
  Cioaba alijiunga na Azam FC Januari mwaka jana akichukua nafasi ya makocha Waspaniola, chini ya Zeben Hernandez Rodriguez na ameshinda taji moja moja tu, Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWAMBUSI ATUA AZAM FC KUWA KOCHA MSAIDIZI WA PLUIJM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top