• HABARI MPYA

  Saturday, June 09, 2018

  MBAO FC YAANZA VYEMA KOMBE LA UHAI, YANGA, AZAM FC, MTIBWA SUGAR ZOTE ZATOA SARE

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  MBAO FC pekee imechomoza na ushindi katika mechi za ufunguzi za Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Mbao ya FC ya Mwanza imeibuka na ushindi wa 1-0, dhidi ya Mbeya City FC, bao pekee la Aman Anuar dakika ya pili katika moja ya mechi nne za ufunguzi za michuano hiyo inayojulikana kama Kombe la Uhai, ikidhaminiwa na Azam TV.
  Mechi nyingine za leo, ambazo zote zimeonyeshwa moja kwa moja na Azam TV, baina na Yanga SC ya Dar es Salaam na Ruvu Shooting ya Pwani, Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Morogoro na Mwadui FC ya Shinyanga na Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma zote zimemalizika kwa sare ya 0-0.
  Kikois cha kwanza cha Mbao FC msimu huu, ambacho wadogo zao leo wameanza vizuri Kombe la Uhai

  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi nne pia, mabingwa watetezi, Simba SC ya Dar es Salaam wakimenyana na Singida United, Tanzania Prisons ya Mbeya na Lipuli FC ya Iringa Saa 8:00 mchana, Stand United ya Shinyanga ikimenyana na Njombe Mji FC na Kagera Sugar ya Bukoba ikimenyana na Ndanda FC Saa 10:00 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBAO FC YAANZA VYEMA KOMBE LA UHAI, YANGA, AZAM FC, MTIBWA SUGAR ZOTE ZATOA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top