• HABARI MPYA

    Thursday, June 07, 2018

    KAGERE AITEKETEZA SINGIDA UNITED NAKURU, NI GOR MAHIA NA SIMBA FAINALI JUMAPILI

    Na Mwandishi Wetu, NAKURU
    MABINGWA watetezi, Gor Mahia ya Kenya watakutana na Simba SC ya Tanzania katika fainali kali ya SportPesa Super Cup Jumapili Uwanja wa Afraha, Nakuru.
    Hiyo ni baada ya Gor Mahia kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida United katika mchezo Nusu Fainali ya pili leo Uwanja wa Afraha, mabao ya Meddie Kagere moja kila kipindi.
    Gor Mahia sasa itakutana na Simba SC ambayo ilishinda kwa penalti 5-4 dhidi ya Kakamega Homeboyz katika Nusu Fainali ya Kwanza baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Afraha pia.

    Waliofunga penalti za Simba SC leo ni viungo, Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomary Kapmbe, Shiza Kichuya na Jonas Mkude, wakati Gor Mahia walipiga juu penalti yao ya mwisho.
    ikumbukwe mchezo wa kwanza pia Simba ilipenya kwa matuta, penalty 3-2 baada ya sare ya 0-0 pia dhidi ya Kariobangi Sharks kabla ya kuendeleza ushindi wa staili hiyo mbele ya Kakamega iliyowatoa Yanga  ya Tanzania pia kwa kuwachapa 3-1.      
    Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Jumapili na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 
    Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500. 
    Bingwa mtetezi ni Gor Mahia ambayo mwaka jana iliifunga AFC Leopards 2-1 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAGERE AITEKETEZA SINGIDA UNITED NAKURU, NI GOR MAHIA NA SIMBA FAINALI JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top