• HABARI MPYA

  Tuesday, June 12, 2018

  HUKO DODOMA KOMBE LA UHAI…SIMBA WATOTO NAO WATOBOLEWA 1-0 NA NJOMBE MJI FC

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  MABINGWA watetezi, Simba SC wamechapwa 1-0 na Njombe Mji FC katika mchezo wa Kundi B Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Kombe la Uhai inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo C viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Bao pekee lililowazamisha Simba SC limefungwa na Kassim Yussuph dakika ya 20, wakati mchezo mwingine wa Kundi B, Stand United imeichapa Singida United 2-1, mabao yake yakifungwa na Tariq Seif dakika ya sita na Morris Haela dakika ya 67 huku la wapinzani wao likifungwa na Said Habib dakika ya 20.
  Hiki ni kikosi cha kwanza cha Simba SC, ambacho wadogo zao leo wamechapwa 1-0 na Njombe Mji FC

  Mechi nyingine za Kombe la Uhai leo zilikuwa ni za Kundi D, Tanzania Prisons wakiikung’uta 3-0 Ndanda FC mabao ya Vedastus Mwimbaji dakika ya 19, Cleophace Mkandala dakika ya 43 na Isaac Kwayawaya dakika ya 68, wakati Lipuli FC imegawana pointi na Kagera Sugar baada ya sare ya 0-0.   
  Ikumbukwe Simba SC ilianza vyema michuano hiya inayoonyeshwa moja kwa moja na Azam TV kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Singida United kwenye mechi yake ya kwanza siku ambayo Stand United iliichapa Njombe Mji FC 1-0, na Kundi D Tanzania Prisons ilishinda 2-0 dhidi ya Lipuli FC na Ndanda FC ikailaza 2-1 Kagera Sugar. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HUKO DODOMA KOMBE LA UHAI…SIMBA WATOTO NAO WATOBOLEWA 1-0 NA NJOMBE MJI FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top