• HABARI MPYA

  Friday, October 20, 2017

  MCHEZAJI 'AUMIA VIBAYA' NA KUTOKWA DAMU NYINGI EUROPA LEAGUE

  NYOTA wa Dynamo Kiev, Domagoj Vida jana alitokwa na damu nyingi kichwani hadi kushindwa kuendelea kucheza baada ya kugongana na kiungo wa Young Boys, Moumi Ngamaleu.
  Nahodha huyo wa klabu hiyo, ambaye anafahamika kwa staili yake uchezaji wa kindava katika Ligi ya Ukraine, ilibidi apatiwe matibabu ya haraka baada ya tukio hilo katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya 2-2.
  Baada ya kutibiwa kwa muda, beki huyo akawastaajabisha wengi kwa kuamua kurudi uwanjani kucheza kwenye mechi hiyo ya Europa League, lakini akalazimika kujitoa baada ya damui kuendelea kuvuja kwa wingi na kupenya kwenye bandeji alizofungwa.

  Beki wa Dynamo Kiev, Domagoj Vida akitokwa damu baada ya kuumia jana katika mchezo dhidi ya Young Boys PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Vida alionekana anayesononeka wakati anaondoka uwanjani, lakini picha za tukio lenyewe zitamuondolea shaka baadaye kwamba alistahili kuondoka. 
  Kichwa chake na jezi yake vililoa damu na kukumbushia picha ya gwiji wa England, Terry Butcher. 
  Ngamaleu pia alipatiwa matibabu akaendelea kidogo na mchezo kabla ya naye kufanyiwa mabasiliko zikiwa zimebaki dakika tano.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI 'AUMIA VIBAYA' NA KUTOKWA DAMU NYINGI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top