• HABARI MPYA

  Saturday, January 20, 2024

  ARSENAL YAICHAPA CRYSTAL PALACE 5-0 EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi  Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Magalhães dakika ya 11, kipa Dean Henderson aliyejifunga dakika ya 37, Leandro Trossard dakika ya 59 na Gabriel Martinelli mawili dakika ya 90+4 na 90+5.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya tatu, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake 21 za mechi 21 nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA CRYSTAL PALACE 5-0 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top