• HABARI MPYA

  Thursday, January 11, 2024

  LIVERPOOL YAICHAPA FULHAM 2-1 CARABAO CUP ANFIELD


  TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup usiku wa jana Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Curtis Jones dakika ya 68 na Cody Gakpo dakika ya 71 kufuatia Willian kuanza kuifungia Fulham dakika ya 19.
  Timu hizo zitarudiana Januari 24 Uwanja wa Craven Cottage Jijini London na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Chelsea na Middlesbrough katika Fainali.
  Mechi ya kwanza Middlesbrough ilishinda 1-0 juzi Uwanja wa Riverside mjini Middlesbrough na timu hizo zitarudiana Januari 23 Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA FULHAM 2-1 CARABAO CUP ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top