• HABARI MPYA

    Saturday, January 06, 2024

    GWIJI WA BRAZIL MARIO ZAGALLO AFARIKI DUNIA AKIWA ANA MIAKA 92


    GWIJI wa soka Brazil, Mário Jorge Lobo Zagallo amefariki dunia Ijumaa Jijini Rio de Janeiro nchini humo akiwa ana umri wa miaka 92 baada ya kuugua kwa muda.
    Gwiji huyo alipelekwa hospitali Rio de Janeiro wakati wa Krisimasi kufuatia kuzidiwa na maradhi kabla ya kuaga Dunia Ijumaa na kifo chake kinamaanisha hakuna tena shujaa wa kikosi cha Brazil aliyekuwemo kwenye kikosi kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 1958 aliye hai. 
    Akiwa mchezaji, Zagallo alikuwa winga mwenye kipaji kikubwa ambaye alishinda Kombe la Dunia mbili, 1958 na 1962, kabla ya kugeukia ukocha ambako pia aliipa Brazil taji hilo mara mbili, mwaka 1970 na 1992.
    Enzi za uhai wake alicheza klabu mbili tu, Flamengo kuanzia 1951 hadi 1958 mechi 217 na kufunga mabao 30, kabla ya kuhamia Botafogo alikocheza kuanzia 1958 hadi 1965 jumla ya mechi 115 na kufunga mabao 46 akifanya jumla ya idadi ya mechi 332 na mabao 76 katika klabu hizo pekee.
    Kwa timu ya taifa ya Brazil alicheza jumla ya mechi 33 na kufunga mabao matano kuanzia mwaka 1958 hadi 1964.
    Zagallo alimuoa Alcina de Castro mwaka 1955 ambaye aliishi naye hadi mwaka 2012 alipofariki dunia wakiwa tayari wana watoto wanne.
    Mungu ampumzishe kwa amani Mário Jorge Lobo Zagallo. Amín.
    Zagallo akiwa na Pele enzi za uhai wao
    Zagallo akiwa na kikosi cha Brazil mwaka 2002
    Zagallo ni wa kwanza kushinda Kombe la Dunia mara mbili kama mchezaji na mara mbili kama Kocha 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GWIJI WA BRAZIL MARIO ZAGALLO AFARIKI DUNIA AKIWA ANA MIAKA 92 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top