• HABARI MPYA

  Wednesday, January 03, 2024

  TAIFA STARS WANAVYOJIFUA CAIRO KUJIANDAA NA AFCON 2024


  WACHEZAJI wa imu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ wakifanya mazoezi Gym katika siku ya pili ya kambi yao Jijini Cairo nchini Misri kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
  Kuelekea Fainali za AFCON zinazotarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11 nchini Ivory Coast, Taifa Stars imeweka kambi katika hoteli ya Reddison Blu Jijini Cairo na inatarajiwa kuondoka Jumatatu kwenda San Pedro, Ivory Coast baada ya mchezo wa kirafiki na Misri Jumapili Uwanja wa Cairo International.
  Taifa Stars imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hizo zikiwa Fainali zao za tatu za AFCON baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri, ambako kote iliitolewa hatua ya makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS WANAVYOJIFUA CAIRO KUJIANDAA NA AFCON 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top