• HABARI MPYA

  Tuesday, January 02, 2024

  YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


  KLABU ya Yanga imefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamus FC ya Sudan Kusini usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Yanga wakitangulia kwa bao la kiungo Farid Mussa Malik dakika ya 16, kabla ya David Vincent kuisawazishia Jamus FC dakika ya 42.
  Shujaa wa Yanga leo ni beki Nickson Clement Kibabage aliyeifungia timu hiyo bao la ushindi dakika ya 90 na ushei na kwa matokeo hayo wanafikisha pointi sita baada ya mechi mbili kufuatia ushindi wa 5-0 dhidi ya Jamhuri kwenye mchezo wa kwanza hapo hapo New Amaan Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top