• HABARI MPYA

  Saturday, January 27, 2024

  MAN CITY YASONGA MBELE KOMBE LA FA, CHELSEA YABANWA DARAJANI


  BAO la beki Mholanzi, Nathan Benjamin Aké dakika ya 88 liliipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur katika mchezo wa Raundi ya Nne Kombe la FA England usiku wa jana Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Wakati Man City inakwenda Raundi ya Tano, mchezo mwingine wa Raundi ya Nne Kombe la FA jana, wenyeji Chelsea ililazimishwa sare ya 0-0 na Aston Villa Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, hivyo timu hizo zitarudiana.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YASONGA MBELE KOMBE LA FA, CHELSEA YABANWA DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top