• HABARI MPYA

  Thursday, January 04, 2024

  KAPTENI MBWANA SAMATTA ARIPOTI KAMBINI TAIFA STARS MISRI


  NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta anayechezea PAOK ya Ugiriki akiwa mazoezini leo Uwanja mdogo wa Cairo International baada ya kuwasili kambini leo kujiunga na wenzake kwa maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
  Fainali za AFCON zinatarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11 mwaka huu nchini Ivory Coast na Taifa Stars imepangwa Kundi F pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Morocco na Zambia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAPTENI MBWANA SAMATTA ARIPOTI KAMBINI TAIFA STARS MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top