• HABARI MPYA

  Monday, January 01, 2024

  AMROUCHE ATEUA 30 KWENDA KAMBINI TAIFA STARS MISRI MANDALIZI YA AFCON


  KOCHA Mkuu wa imu ya taifa, Taifa Stars, Mualgeria Adel Amrouche ameteua wachezaji 30 kuingia kambini nchini Misri kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11 nchini Ivory Coast.
  Taifa Stars ambayo imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeondoka leo Dar es Salaam kwenda Cairo, Misri kuweka kambi ya wiki moja kabla ya kwenda Ivory Coast.
  Kwa Taifa Stars hizo zitakuwa Fainali za tatu za AFCON kucheza baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri, kote wakitolewa hatua ya makundi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMROUCHE ATEUA 30 KWENDA KAMBINI TAIFA STARS MISRI MANDALIZI YA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top