// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PAMBA FC YAPIGA HONI LIGI KUU, YACHAPA STAND 4-1 NYAMAGANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PAMBA FC YAPIGA HONI LIGI KUU, YACHAPA STAND 4-1 NYAMAGANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Sunday, January 21, 2024

  PAMBA FC YAPIGA HONI LIGI KUU, YACHAPA STAND 4-1 NYAMAGANA


  WENYEJI, Pamba FC jana waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mwana Stand United katika mchezo wa Ligi ya NBC Champonship Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
  Mabao ya Pamba FC yalifungwa na Mudathir Said, Hassan Mwasapili, Haruna Chanongo na Lazaro Mlingwa, wakati bao pekee la Stand United lilifungwa na Lucas Sesana. 
  Mechi nyingine za jana za Ligi ya NBC Championship, Mbuni FC iliichapa Pan Africans mabao 3-1 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijjini Arusha na Mbeya City ikawatandika Mbeya Kwanza 4-2 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Ligi ya NBC Championship itaendelea leo kwa michezo mingine mitatu; TMA na Cosmopolitan Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, COPCO na Biashara United Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Ken Gold na Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
  Msimamo wa NBC Championship ni Pamba FC kileleni pointi 40 mechi 18, ikifuatiwa na Ken Gold pointi 39 mechi 17.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMBA FC YAPIGA HONI LIGI KUU, YACHAPA STAND 4-1 NYAMAGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top