// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI KWA MATUTA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI KWA MATUTA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, January 10, 2024

  SIMBA SC YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI KWA MATUTA


  TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada y ushindi wa penalti 3-2 dhidi ya Singida Fountain Gate leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Singida Fountain Gate ilitangulia kwa bao la mshambuliaji Mkenya Elvis Rupia dakika ya 11, kabla ya kiungo Mkongo Fabrica Luamba Ngoma kuisawazishia Simba SC dakika ya 90 na ushei.
  Na kwenye mikwaju ya penalti kipa wa Simba SC, Ali Salim aliyeokoa penalti za mabeki Gardiel Michael, Hamad Waziri na mshambuliaji Mnyarwanda Meddie Kagere kuipa Simba tiketi ya Fainali Kombe la Mapinduzi.
  Waliofunga penalti za Simba ni viungo Luis Jose Miquissone, raia wa Msumbiji, Israel Patrick Mwenda na Moses Phiri, wakati ya Shomari Kapombe iliokolewa na ya Mrundi, Saido Ntibanzokiza ikagonga mwamba wa juu na kwenda nje.
  Ni viungo, Mkenya Duke Abuya na mzawa, Deus Kaseke pekee waliofunga upande wa Singida Fountain Gate.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top