• HABARI MPYA

  Thursday, January 18, 2024

  DRC NA ZAMBIA HAKUNA MBABE, SARE 1-1 SAN PEDRO


  MECHI za kwanza za hatua ya makundi Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zimekamilishwa jana kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Zambia katika mchezo wa Kundi F Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro nchini Ivory Coast.
  Zambia walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na kiungo wa Red Star Belgrade ya Serbia, Kings Kangwa dakika ya 23, kabla ya kiungo wa Brentford ya England, Yoane Wissa Bileko kuisawazishia DRC dakika ya 27.
  Morocco iliyoifunga Tanzania 3-0 katika mchezo wa kwanza jana ndio inaongoza Kundi F kwa pointi zake tatu, ikifuatiwa na DRC na Zambia zenye pointi moja kila moja, wakati Taifa Stars inashika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DRC NA ZAMBIA HAKUNA MBABE, SARE 1-1 SAN PEDRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top