• HABARI MPYA

  Monday, January 01, 2024

  SIMBA SC YAANZA VIZURI KOMBE LA MAPINDUZI, YASHINDA 3-1


  TIMU ya Simba SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKU katika mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mabao ya Simba leo yamefungwa na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri dakika ya nane, beki Mohamed Hassan dakika ya 64 aliyejifunga akijaribu na kuokoa krosi ya kiungo wa Msumbiji, Luis Miquissone na kiungo mpya, Saleh Karabaka dakika ya 65, wakati bao la JKU limefungwa na Neva Kaboma dakika ya 42.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAANZA VIZURI KOMBE LA MAPINDUZI, YASHINDA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top