• HABARI MPYA

  Sunday, January 07, 2024

  YANGA SC YATUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI


  TIMU ya Yanga SC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa mabao 3-1 na APR ya Rwanda katika mchezo wa Robo Fainali usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mabao ya APR yamefungwa na Soulei Sanda dakika ya 45 na ushei, Mbaoma Víctor kwa penalti dakika ya 49 na Sharaf Eldin Shaiboub dakika ya 79 baada ya winga Mkongo, Jesús Moloko kuanza kuifungia Yanga dakika ya 23.
  Sasa APR itakutana na mabingwa watetezi, Mlandege SC katika mchezo wa Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top