• HABARI MPYA

  Tuesday, January 16, 2024

  SIMBA SC YAWATEMA NA BALEKE NA PHIRI PIA


  KLABU ya Simba imeachana na washambuliaji wake wawili wa kigeni, Mkongo Jean Othos Baleke na Mzambia, Moses Phiri, hivyo kufanya jumla ya wachezaji sita iliyowaondoa dirisha hili dogo.
  Wengine ni wazawa viungo Jimson Stephen Mwanuke (24), Nassor Yahaya Kapama (27) na washambuliaji Shaaban Iddi Chilunda (25) na Mohamed Mussa Saleh (22).
  Ikumbukwe Simba imesajili wachezaji watano wapya dirisha hili dogo wakiwemo viungo wawili, Msenegal Babacar Sarr (26) kutoka US Monastir ya Tunisia na winga, Ladaki Juma Chasambi (19) kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  Wengine wote ni washambuliaji, Muivory Coast Freddy Michael Kouablan (25) kutoka Green Eagles ya Zambia ambako alikuwa anaongoza kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo, Mgambia, Pa Omar Jobe (25) kutoka Zhenis ya Kazakhstani na Saleh Karabaka Kikuya (23) kutoka JKU ya Zanzíbar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWATEMA NA BALEKE NA PHIRI PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top