• HABARI MPYA

  Monday, January 01, 2024

  SINGIDA WAICHAPA APR 3-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


  TIMU ya Singida Fountain Gate imefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya APR ya Rwanda leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mabao ya Singida Fountain Gate yamefungwa na mshambuliaji Mkenya, Elvis Rupia dakika ya 45 na ushei kwa penalti, kiungo Mnigeria Morice Chukwu dakika ya 76 na mshambuliaji Mkongo, Francy Kazadi dakika ya 86, baada ya APR kutangulia na bao la mshambuliaji Mnigeria Mbaoma Víctor dakika ya pili tu.
  Singida Fountain Gate wanafikisha pointi sita na moja kwa moja wanajihakikishia kwenda Robó Fainali ya michuano hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA WAICHAPA APR 3-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top