• HABARI MPYA

  Wednesday, January 17, 2024

  TAIFA STARS PUNGUFU YACHAPWA 3-0 NA MOROCCO AFCON


  TANZANIA imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi F usiku huu Uwanja wa Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro, Ivory Coast. 
  Mabao ya Simba wa Atlasi yamefungwa na beki wa Al-Shabab ya Saudí Arabia, Romain Ghanem Paul Saïss dakika ya 30, kiungo wa Marseille ya Ufaransa, Azzedine Ounahi na mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri dakika ya 80.
  Taifa Stars ilimaliza pungufu baada ya kiungo wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine Novatus Dismas Miroshi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS PUNGUFU YACHAPWA 3-0 NA MOROCCO AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top