• HABARI MPYA

    Sunday, January 21, 2024

    MALI YAITOA MAURITANIA AFCON, BURKINA FASO SARE NA ALGERIA 2-2


    TIMU ya taifa ya Angola jana imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu Hatua ya Mtoano Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mauritania katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa La Paix mjini Bouaké, Ivory Coast. 
    Mabao ya Angola yalifungwa na washambuliaji Gelson Dala wa Al Wakrah ya Qatar mawili dakika ya 30 na 50 na Deivi Miguel Vieira 'Gilberto' wa Petro de Luanda ya kwao dakika ya 53, wakati ya Mauritania yalifungwa na washambuliaji pia, Sidi Amar wa Nouadhibou ya kwao na Aboubakary Koita wa Sint-Truiden ya Ubelgiji.
    Mechi nyingine ya Kundi D jana, Algeria ilitoka sare ya 2-2 Burkina Faso hapo hapo Uwanja wa La Paix mjini Bouaké.
    Mabao ya Burkina Faso yalfungwa na washambuliaji Mohamed Konaté wa Akhmat Grozny ya Urusi dakika ya 45 na Bertrand Traoré wa Aston Villa dakika ya 71 kwa penalti, wakati ya Algeria yalifungwa na mshambuliaji wa Al Sadd ya Qatar,Baghdad Bounedjah yote dakika ya 51 na 90 na ushei.
    Kwa matokeo hayo, Angola na Burkina Faso zinafikisha pointi nne zikiongoza Kundi D mbele ya Algeria yenye pointi mbili na Mauritania haina pointi na itakamilisha mechi zake kwa kumenyana na  Algeria.
    Mechi ya Kundi E jana Tunisia ilitoa sare ya 1-1 na Mali Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo. Mshambuliaji wa Auxerre ya Ufaransa, Lassine Sinayoko alianza kuifungia Mali dakika ya 10, kabla ya kiungo wa Lecce ya Italia, Hamza Rafia kuisawazishia Tunisia dakika ya 20.
    Mali inaendelea kuongoza Kundi E kwa pointi zake nne, ikifuatiwa Namibia pointi tatu, Tunisia yenye pointi moja, wakati Afrika Kusini haina pointi mkiani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALI YAITOA MAURITANIA AFCON, BURKINA FASO SARE NA ALGERIA 2-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top