• HABARI MPYA

  Wednesday, January 03, 2024

  SIMBA QUEENS YAENDELEZA UTEMI KWA YANGA PRINCESS


  TIMU ya Simba Queens imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya watani wao, Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Aisha Mnuka mawili na Mkenya Vivian Corazone, wakati la Yanga Princess limefungwa na Neema Paul.
  Kwa ushindi huo, Simba Queens inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza Ligi ya Wanawake kwa pointi tatu zaidi ya watani wao bao, Yanga Princess baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YAENDELEZA UTEMI KWA YANGA PRINCESS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top