• HABARI MPYA

    Tuesday, January 16, 2024

    SIMBA SC YAWAACHA WANNE KWA MIPIGO WAMO CHILUNDA NA MWANUKE


    KLABU ya Simba imeachana na wachezaji wake wanne, viungo Jimson Stephen Mwanuke (24), Nassor Yahaya Kapama (27) na washambuliaji Shaaban Iddi Chilunda (25) na Mohamed Mussa Saleh (22).
    Ikumbukwe Simba imesajili watano wapya dirisha hili dogo wakiwemo viungo wawili, Msenegal Babacar Sarr (26) kutoka US Monastir ya Tunisia na winga, Ladaki Juma Chasambi (19) kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
    Wengine wote ni washambuliaji, Muivory Coast Freddy Michael Kouablan (25) kutoka Green Eagles ya Zambia ambako alikuwa anaongoza kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo, Mgambia, Pa Omar Jobe (25) kutoka Zhenis ya Kazakhstani na Saleh Karabaka Kikuya (23) kutoka JKU ya Zanzíbar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAWAACHA WANNE KWA MIPIGO WAMO CHILUNDA NA MWANUKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top