• HABARI MPYA

  Thursday, January 04, 2024

  RAIS WA YANGA AKUTANA NA RAIS WA PSG UFARANSA


  RAIS wa Yanga SC na Mwenyekiti wa Chama cha Klabu za Soka (ACÁ), Afrika, Hersi Ally Said amekutana na Rais wa Paris Saint-Germain, Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi,
   ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu za Ulaya Jijini Paris, Ufaransa jana.
  Hersi alipewa mwaliko maalum na Nasser Bin Ghanim Al-Khelaifi kwa lengo la kujadili jinsi vyama hivyo vikubwa vinavyoweza kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya klabu.
  Aidha,  Nasser Bin Ghanim Al- Khelaifi alimkaribisha Hersi kushuhudia mchezo wa Fainali ya Trophée des Champions uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc de Prince, ambao PSG ilibeba taji hilo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toulouse.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS WA YANGA AKUTANA NA RAIS WA PSG UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top