• HABARI MPYA

  Monday, January 15, 2024

  MAN UNITED YAAMBULIA SARE KWA SPURS, 2-2 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United jana wametoa sare ya kufungana mabao 2-2 na Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na washambuliaji Mdenmark, Rasmus Højlund dakika ya tatu na Muingereza, Marcus Rashford dakika ya 40, wakati ya Spurs yamefungwa na Richarlison dakika ya 19 Rodrigo Bentancur dakika ya 46.
  Kwa matokeo hayo, Tottenham Hotspur inafikisha pointi 40 ingawa inabaki nafasi ya tano, wakati Manchester United inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya saba baada ya wote kucgeza mechi 21.
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAAMBULIA SARE KWA SPURS, 2-2 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top