• HABARI MPYA

    Friday, January 19, 2024

    SALAH AUMIA, MISRI YADROO NA GHANA, NIGERIA YAIZIMA IVORY COAST


    WAKATI Nigeria imeweka hai matumaini ya kwenda Hatua ya Mtoano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu zinazoendelea nchini Ivory Coast, Ghana imejiweka njia panda.
    Nigeria ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ivory Coast katika mchezo wa Kundi A jana Uwanja Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan bao la mkwaju wa penalti la beki wa PAOK ya Ugiriki, William Paul Troost-Ekong dakika ya 56.
    Mechi nyingine ya Kundi A jana, Equatorial Guinea ilishinda 4-2 dhidi ya Guinea-Bissau hapo hapo Uwanja Olympique Alassane Ouattara.
    Sasa Equatorial Guinea wanaongoza Kundi A kwa wastani wa mabao dhidi ya Nigeria wote wakiwa na pointi nne, Ivory Coast pointi tatu nafasi ya tatu na Guinea-Bissau inashika mkia haina pointi.
    Mchezo pekee wa Kundi B jana ulimalizika kwa sare ya 2-2 baina ya Misri na Ghana Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan.
    Mabao ya Ghana yalifungwa na winga Mohammed Kudus wa West Ham United ya England yote dakika ya 45 na 71, wakati ya Misri yalifungwa na washambuliaji, Omar Marmoush wa Eintracht Frankfurt ya Ujerumani dakika ya 69 na Mostafa Mohamed wa Nantes ya Ufaransa dakika ya 74.
    Misri ilipata pigo baada ya Nahodha wake, Mohamed Salah wa Liverpool ya England kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na mshambuliaji wa Pyramids ya nyumbani, Misri Mostafa Fathi dakika ya 45.
    Cape Verde ambayo leo inacheza na Msumbiji inaendelea kuongoza Kundi A kwa pointi zake tatu ikifuatiwa na Misri pointi mbili, Ghana pointi moja sawa na Mambas.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAH AUMIA, MISRI YADROO NA GHANA, NIGERIA YAIZIMA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top