• HABARI MPYA

  Wednesday, January 03, 2024

  SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


  TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Kundi B usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
  Mabao ya Wekundu wa Msimbazi yamefungwa na viungo washambuliaji, Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana dakika ya 47 na Luis Jose Miquissone wa Msumbiji dakika ya 59 na kwa ushindi huo Simba inafikisha pointi sita katika mchezo wa pili sawa na Singida Fountain Gate iliyocheza mechi zote tatu za Kundi B.
  Mechi ya Kundi B iliyotangulia jioni, APR ilishinda 3-1 dhidi ya JKU hapo hapo New Amaan Complex.
  Mabao ya APR yalifungwa na Niyibizi  Ramadhani mawili dakika ya saba na 67 na Mbaoma Víctor dakika ya 47, huku la JKU likifungwa na Saleh Abdallah dakika ya 45 na ushei.
  Simba SC ndio inaongoza sasa kundi hilo kwa wastani wa mabao, ikifuatiwa na Singida, wakati APR yenye pointi tatu za mechi mbili ni ya tatu na JKU inashika mkia ikiwa haina pointi na imeaga mashindano baada ya kukamilisha mechi zake tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top