• HABARI MPYA

  Thursday, January 11, 2024

  MAYELE NA AZIZ KI WAKUTANA ABU DHABI BURKINA FASO IKIICHAPA DRC 2-1


  NYOTA Mburkinabe wa Yanga, Stephane Aziz Ki (kulia) akiwa na nyota wa Pyramids ya Misri, Mkongo Fiston Kalala Mayele baada ya mchezo wa kirafiki baina ya timu zao za taifa kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) jana Uwanja wa Baniyas Jijini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE).
  Burkina Faso ilishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Ibrahim Blati Toure dakika ya 36 na Mohamed Konate dakika ya 41, huku bao pekee la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) likifungwa na Chancel Mbemba dakika ya 56.
  Ikumbukwe msimu uliopita Mayele alikuwa pamoja na Aziz Ki katika klabu ya Yanga wakishinda mataji yote matatu ya nyumbani na kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE NA AZIZ KI WAKUTANA ABU DHABI BURKINA FASO IKIICHAPA DRC 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top